History
Icon-add-to-playlist Icon-download Icon-drawer-up
Share this ... ×
...
By ...
Embed:
Copy
460>_632236

Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika ni mojawapo ya idhaa za nje zinazosikilizwa sana Tanzania. Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili Emmanuel Muganda anatuelezea jinsi idhaa hiyo inavyofanya kazi. Je idhaa hiyo ilianzishwa lini? Nini yalikuwa mdhumuni ya kuianzisha? Ni Radio gani Tanzania zinazorusha matangazo yao? Je nini maoni yake juu ya dhana moya ya uandishi wa raia? Je Africa ina nafasi gani katika teknolojia mpya ya habari na mawasiliano?

http://www.voanews.com/swahili/

[PLAY]
460>_632237

Mheshimiwa Mhonga Said Rhuwanya ni mmoja wa wabunge vijana wanaokuja juu. Akiwa na umri wa miaka 26 aliwashangaza wengi alipochaguliwa na CHADEMA kuwa Mbunge Viti Maalum. Huko Bungeni amekuwa ni mmoja wa wabunge vijana walio makini na waliojikita kuikomboa nchi yetu Je Mheshimiwa Mhonga ametokea wapi? Ni sababu gani zilimfanya aingie kwenye siasa? Kwa nini alijiunga na CHADEMA?

[PLAY]
460>_632238

Tausi Likokola sio jina geni kwa wa-Tanzania wengi. Mwanamitindo huyu ameshafanya kazi na designers wakubwa kama GUCCI, Escada, Tommy Hilfiger, Christian Dior na Issey Miyake. Lakini Tausi hajaishia kwenye mitindo peke yake bali anafanya kazi kubwa kuisadia jamii aliyotoka. Je Tausi Likokola katokea wapi? Nini kilifanya aitwe Goodwill Ambassador wa Tanzania? Nini kilimuingiza kwenye mitindo? Je ana ushauri gani kwa wasishana wanaotaka kuwa wanamitindo kama yeye?

Tembelea tovuti zake:
www.TausiDreams.com , www.TausiAidsFund.org

[PLAY]
460>_632239

Mheshimiwa Kleist Sykes, ambae ni mtoto wa marehemu Abdulwahid Sykes anaongelea mchango wa familia ya Sykes kwenye uhuru wa Tanganyika na kitabu cha Mohamed Said. Je nini maoni yake juu ya kitabu cha The Life and Times of Abdulwahid Sykes? Je alimpa ushauri gani Mohamed Said? Je kuna ukweli wowote kuwa waislam ndio peke yako waliongoza harakati za uhuru? Je atapenda watanzania wamkumbuke vipi Mzee Abdul Sykes?

[PLAY]
460>_632240

Katika kitabu chake cha "The life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968): The untold story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika" mwandishi Mohamed Said anaangalia mchango wa waislam katika harakati za kuleta uhuru wa Tanganyika. Je waislam ndio walioanzisha TAA na TANU? Je ni kweli Mwalimu Nyerere alinyakua TANU toka kwa waislam na kukifanya kuwa chombo cha kanisa? Nani alisaidia sana kuleta uhuru wa Tanganyika kati ya Mwalimu Nyerere na Abdul Sykes? Sikiliza zaidi.

[PLAY]
460>_632241

Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ni mmoja wa wabunge vijana machachari na maarufu kwenye siasa ya Tanzania. Akiwa na umri wa miaka 30 tu, Mheshimiwa Zitto Kabwe ni mbunge kijana kuliko wabunge wote wa kuchaguliwa. Je Zitto Kabwe ametokea wapi? Yupo wapi? Anaelekea wapi? Kwa nini aliingia kwenye siasa? Je ana matatizo gani Mheshimiwa Spika? Je wapinzani wana imani na Spika? Je ni kweli ana mpango wa kuhama CHADEMA na kuhamia CCM?

[PLAY]
460>_632242

Mheshimiwa Amina Chifupa Mpakanjia ni mmoja wa wanasiasa chipukizi wanaokuja juu sana kwenye siasa ya Tanzania. Akiwa na umri wa miaka 25 tu ameweza kuwashangaza watu wengi kwa mambo makubwa anayoyafanya. Je Mh. Amina Chifupa ametokea wapi? Kwa nini aliingia kwenye siasa? Nani alimshauri? Kwa nini kawavalia njuga wauza madawa ya kulevya? Je ana ndoto za kuja kugombea urais hapo baadae?

[PLAY]
460>_632243

Mheshimiwa Augustine Lyatonga Mrema ni mmoja wa wanasiasa maarufu nchini Tanzania. Lakini hivi sasa umaarufu wake umeanza kupungua kwa kasi kubwa na watu wengi wanamuona kama kaporomoka kisiasa. Je Mrema ametoka wapi? Yupo wapi na anaelekea wapi? Ni sababu gani zilimtoa CCM na NCCR-MAGEUZI? Je ni kweli Mrema kapandikizwa na CCM ili kuua upinzani? Na vipi kuhusu shahada yake? Sikiliza zaidi.

[PLAY]
460>_632244

Bara la Afrika lina kila kitu kuanzia ardhi kubwa yenye rutuba, maziwa makubwa, mito, madini, mazao na mbuga za wanyama. Vilevile ni bara la pili kwa ukubwa na inasemekana binadamu wa kwanza aliishi huko. Pia ni bara linaloongoza kwa kupewa misaada na nchi nyingine. Lakini na mambo yote hayo Afrika ni bara linaloshika nafasi ya mwisho kwenye masuala mengi ya maendeleo? Je tatizo ni nini? Utumwa? Ukoloni? Ukoloni mamboleo? Dr. Malima Bundara mwandishi wa kitabu cha “Waafrika Ndivyo Walivyo?” anasema tatizo ni Waafrika wenyewe. Sikiliza zaidi.

[PLAY]
460>_632245

Teknolojia ya habari na mawasiliano imebadilisha jinsi binadamu tunavyoishi. Mabadiliko haya yamempa nguvu kubwa sana mtu wa kawaida. Leo hii watu wa kawaida wanaweza kumiliki vyombo vyao vya habari bila hata kulipia gharama kubwa. Mwanahabari na Mwanablogu Ndesanjo Macha(Pichani kulia akiwa na Issa Michuzi) anatuelezea vizuri juu ya dhana mpya ya uandishi wa raia. Je blogu ni nini? Nini faida za kuwa na blogu? Je Afrika tuna nafasi gani katika hii teknolojia mpya? Kiswahili kina nafasi gani? Sikiliza zaidi.

Tembelea blogu ya Ndesanjo Macha:
www.jikomboe.com

[PLAY]

Next Page