October 22, 2006 05:38 PM PDT
Josiah Kibira ni mtengeneza sinema wa ki-Tanzania anaeishi kwenye jimbo la Minesotta, Marekani. Jina lake si geni kwa wa-tanzania wengi. Filamu zake alizotengeneza na zikapata umaarufu ni BongoLand na Tusamehe. Je Bw. Kibira ametokea wapi? Yupo wapi na anaelekea wapi? Je hizi filamu zake zina ujumbe gani kwa wa-Tanzania? Ni kwa nini anatumia lugha ya Kiswahili kwenye hizi filamu? Je Bwana Kibira ana mpango wa kutengeneza filamu gani nyingine kuhusu Tanzania?
Unaweza kutembelea tovuti ya Kibira Films International:
www.kibirafilms.com
October 14, 2006 11:03 AM PDT
Leo 10/14/2006 miaka 7 tangia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere atutoke. Je Wa-Tanzania tunatakiwa kumkumbuka vipi Mwalimu Nyerere? Nchi yetu Tanzania inaelekea wapi? Je kwa nini familia ya Mwalimu Nyerere haijuhusishi na siasa hivi sasa? Je kwa nini familia ya Mwalimu ilipinga vikali ule muswada wa kumuenzi Mwalimu na kuchukua mali zake zote na kuzifanya za serikali? Je familia ya Mwalimu inafanya shughuli gani kumuenzi? Sikiliza zaidi.
October 08, 2006 06:19 AM PDT
John Mnyika ni mmoja wa vijana wanaokuja juu kwenye siasa za Tanzania.Akiwa na umri wa miaka 26 tu ameweza kushangaza wengi katika ulimwengu wa siasa.Mwaka jana aligombania kiti cha Ubunge kwenye jimbo la Ubungo na makali yake yalionekana.Watu wengi waliomsikia au walio karibu nae wanasema John Mnyika ndio atakuja kuwa mkombozi wa Tanzania. Je Bw. Mnyika ametokea wapi? Yuko wapi na anaelekea wapi? Anaongozwa na falsafa gani? Kwa nini ameingia katika siasa? Kwa nini alijiunga na CHADEMA?
Tovuti ya CHADEMA
www.chadema.net
September 30, 2006 08:02 PM PDT
Ni Jumamosi 09/30/2006 Je nini kinaendelea huko Detroit, Michigan? Pesa za kusafirisha miili kwenda nyumbani imepatikana? Je ubalozi ulisaidia gharama zozote? Je ni kweli Rais Kikwete alisema serikali itagharamia usafirishaji? Je kuna mtu yoyote kakamatwa kutokana na haya mauaji? Kisa kilikuwa ni nini? Sikiliza mahojiano niliyofanya na Mheshimiwa Ayub Mfinanga, ambae ni Mwenyekiti wa chama cha Wa-Tanzania huko Michigan.
http://home.insight.rr.com/duesville/waltermazula.htm
September 24, 2006 01:33 PM PDT
Habari kutoka huko Detroit, Michigan zinasema watanzania wawili Walter Mazula na mwenzake Vonetha Nkya wameuwawa kikatili.Mipango ya kusafirisha miili yao bado inaendelea na msaada wako unahitajika.Unaweza kupitia hii tovuti ku sign kitabu cha rambi rambi na kupata habari zaidi:
http://home.insight.rr.com/duesville/waltermazula.htm
September 16, 2006 05:49 AM PDT
Mwalimu Nyerere alishawahi kusema "Tanzania itajengwa na wenye moyo." Moyo huyo sasa unaonyeshwa na Alumni wa shule ya msingi ya Mlimani. Hawa Alumni wameanzisha Organization itakayokuwa inafanya mambo makubwa kwenye shule yao ya zamani.Je nini madhumuni ya kuanzisha hii Organization? Wana mpango wa kufanya miradi gani? Pesa watatoa wapi ya kusaidia shule yao? Kwa nini wanaona ni haki yao kuisaidia hii shule na sio kuiachia serikali? Sikiliza zaidi.
Unaweza kutembelea tovuti yao:
http://www.mlimani.org
September 09, 2006 04:34 AM PDT
Model Cynthia Masasi ni mmoja wa watanzania waliopata mafanikio makubwa sana huko Marekani.Ameweza kutokea kwenye music videos zinazotingisha hapa Marekani na pia kwenye magazeti mbali mbali.Yumo kwenye music videos za wanamuziki maarufu kama Nelly, T.I, Young Joc, Trina, Trick Daddy, Burbba Sprax na Ying Yang Twins.Lakini je Cynthia Masasi ametokea wapi? Yupo wapi na anataka kwenda wapi? Kitu gani kilimfanya awe model?Amepataje haya mafanikio? Ana ushauri gani kwa wengine? Je Cynthia anataka kumpa Rais Kikwete zawadi gani? Kalenda yake inatoka lini?Sikiliza zaidi.
Mnaweza kumtembelea Cynthia Masasi kwenye tovuti yake:
http://www.cynthiamasasi.com
September 02, 2006 06:26 AM PDT
Mwisho wa juma hili nilipata bahati ya kufanya mahojiano na Professor Joseph Mbele ambae ni mwandishi wa kitabu maarufu hapa Marekani kinachoitwa Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Professor Mbele kwa sasa anaishi huko NorthFiled Minnesota ambako anafundisha St. Olaf College tangia mwaka 1991.Kwenye kitabu chake ameelezea kiundani tofauti kati ya utamaduni wa Wamarekani na Waafrika.Je ni vitu gani waafrika inapaswa kujifunza toka kwa wamarekani? Je kuna uwiano wowote kati ya hizi tamaduni mbili? Je ni nini tatizo kati ya Waafrika na Wamarekani weusi? Sikiliza zaidi.
Unaweza kununua kitabu hapa:
www.lulu.com/content/105001
Professor Mbele website:
http://www.africonexion.com/
August 25, 2006 05:18 AM PDT
Cosmas Chidumule anafahamika kwa wengi kama Gwiji la Muziki wa Tanzania.Ni mtunzi na muimbaji wa vibao vingi vilivyopata umashahuri kwenye ulimwengu wa muziki.Baadhi ya vibao mashuhuri ni kama Neema, usitumie pesa kama fimbo, kifo na nalala kwa taabu. Pia ameimba na bendi nyingi mashuhuri kama butiama jazz, Vijana Jaz, Super Matimila, Dar International, Mlimani Park na wana Ndekule.Lakini hivi sasa Cosmas Chidumule ni mtu tofauti? Amebadilisha maisha yake kabisa. Je huyu Gwiji la Muziki ametokea wapi? Yuko wapi? Anaenda wapi? Kwa nini ameokoka? Nini kilitokea hadi kubadilisha maisha yake? Nini maoni yake juu ya muziki wa kizazi kipya Bongo Flava? Sikiliza zaidi.
August 19, 2006 09:11 AM PDT
Ukimwi umekuwa ni tishio kubwa barani Africa. Nchi nyingi zimejitahidi kupambana na ugonjwa huu hatari na zimeweza kufanikiwa. Lakini Tanzania imebakia kuwa ni mojawapo ya nchi zenye wagonjwa wengi wa ukimwi duniani. Je tunatakiwa kufanya nini ili kupambana na huu ugonjwa? Serikali yetu inafanya mambo ya kutosha ili kuutokomeza huu ugonjwa? Uganda waliwezaje kupunguza huu ugonjwa kwa asilimia kubwa? Msikilize Profesa Kilonzo wa hospitali ya Muhimbili akiongea toka Toronto, Canada ambako alikuwa akihudhuria International Aids Confrerence iliyofanyika kuanzia August 13th - 18th.