Mwishoni wa week hii nilipata bahati ya kufanya mahojiano na mwandishi wa habari na mpiga picha maarufu wa gazeti la Daily News/Sunday News Bw. Muhidin Issa Michuzi.Nilimuuliza maswali mengi kuanzia jinsi alivyoanza kazi yake, blog yake, uhuru wa vyombo vya habari nchini, kuvuliwa uraia kwa waandishi wa habari kama Jenerali Ulimwengu na Ali Nabwa, maoni yake kwa ujumla kuhusu Rais Kikwete na mengineyo mengi.Je Bw Michuzi anategemea kuingia kwenye uringo wa siasa? Sikiliza zaidi.
Unaweza pia kumtembelea Bw Michuzi kwenye photo blog:
http://issamichuzi.blogspot.com/

![[PLAY]](http://butiama.podOmatic.com/img/play_button.gif)


