Player_logo Podcasts Community Create a Podcast
460>_632256

Mwishoni wa week hii nilipata bahati ya kufanya mahojiano na mwandishi wa habari na mpiga picha maarufu wa gazeti la Daily News/Sunday News Bw. Muhidin Issa Michuzi.Nilimuuliza maswali mengi kuanzia jinsi alivyoanza kazi yake, blog yake, uhuru wa vyombo vya habari nchini, kuvuliwa uraia kwa waandishi wa habari kama Jenerali Ulimwengu na Ali Nabwa, maoni yake kwa ujumla kuhusu Rais Kikwete na mengineyo mengi.Je Bw Michuzi anategemea kuingia kwenye uringo wa siasa? Sikiliza zaidi.

Unaweza pia kumtembelea Bw Michuzi kwenye photo blog:
http://issamichuzi.blogspot.com/

[PLAY]
460>_632257

Katika hotuba yake kwa wazee wa Mwanza, Rais Jakaya M. Kikwete aliishambulia vikali filamu ya Darwin's Nightmare iliyotengenezwa na rais wa Ufaransa Hubert Sauper. Rais Kikwete aliendelea na kusema "Filamu hii imejaa uzushi na uongo wenye lengo la kupaka matope Tanzania na kuhujumu biashara ya samaki katika ziwa Victoria upande wa Tanzania. Je ni yupi alie sahihi Rais Kikwete au Hubert Sauper? Sikiliza maoni yangu na ya msikilizaji wetu Kennedy Opulukwa ambae ni mwenyeji wa Mwanza.

460>_736900

Mtanzania Joanna Ngwilizi Mbilikira anaeishi Wichitta, Kansas ameomba msaada hospitalini anakofanya kazi na kupewa vitanda 30 ili avipeleke Tanzania.Kuna mtanzania John Owenya ame contact The Guardian na ubalozi wetu na kulalamika na kusema kuwa Joana alidanganya kuhusu hali ya sekta ya afya nchini wakati anaandika proposal ya kuomba huo msaada.Sikiliza maoni yangu upate habari kamili.

[PLAY]

Previous Page  |